[Free Access] Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Mbowe kuachiwa huru, na tafsiri pana ya mwaliko aliopewa Ikulu kwa maongezi na Mama Samia
Utangulizi:
Jana, Machi 4, 2022, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alitangaza nia ya kutoendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mheshimiwa Freeman Mbowe na wenzake watatu ambao walikuwa wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mohamed Ling'wenya, Halfan Bwire na Adam Kasekwa. Uamuzi huo kisheria unaitwa “nolle prosequi.”