Uchambuzi wa kiintelijensia: tuhuma za Bashite kuwa kuna mawaziri wanalipa watu wamtukane Mama Samia ni za kweli au porojo? Ni tuhuma zake kweli au katumwa? Mabadiliko kabineti ya Mama yanukia
Kwa mara nyingine, Bashite ametawala anga za habari kufuatia tuhuma nzito alizotoa jana huko Arusha kwa Mama Samia wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri Mkuu wa zamani marehemu Edward Sokoine.
Tuhuma hizo za Bashite ni kama alivyotamka kwenye video hii
Uchambuzi huu wa kiintelijensia unajikita katika maeneo yafuatayo
Je tuhuma za Bashite kuwa kuna viongozi wakiwemo mawaziri wanalipa watu mtandaoni ili wamtukane Mama Samia ni za kweli au ni uzushi tu wa Bashite?
Kama tuhuma hizo ni za kweli, viongozi/mawaziri husika ni akina nani?
Kama tuhuma ni uzushi, motive ya Bashite ni ipi, na kubwa zaidi ujasiri wa kumdanganya Rais anautoa wapi?
Kama tuhuma ni za kweli, je Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa haifahamu kuhusu hilo au ilifahamu lakini ikamficha Rais?
Bila kujali tuhuma ni za kweli au la, je Bashite alitoa maneno hayo kutoka nafsini mwake au alitumika tu kama kipaza sauti?
Kama alitumika, nani aliyemtuma?
Uchambuzi huu utaangalia pia “wider implications” za tukio la jana ikiwa ni pamoja na taarifa za uwepo wa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, lakini kubwa zaidi, kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu hapo mwakani.