Ujio wa Lissu Januari 25: Mtihani wa kwanza kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa, Said Masoro
Makamu mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ametangaza kurudi nyumbani Januari 25 mwaka huu.
Hii ni mara ya pili kwa Lissu kutangaza kurudi nyumbani, ambapo mwaka jana alieleza kuwa yeye na kiongozi mwingine wa chama hicho aliyepo hifadhini nchini Canada, Godbless Lema, wangerudi mnamo mwezi Machi 2022.
Kurudi kwa Lissu kutakuwa tukio la kwanza kubwa la kisiasa kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa, Said Masoro, aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu mapema mwezi huu, kufuatia kung’olewa kwa mtangulizi wake Diwani Athumani.
Makala hii ya kiintelijensia inachambua ujio huo wa Lissu kama mtihani wa kwanza kwa Masoro katika wadhifa wake huo mpya, hasa ikizingatiwa kuwa mara kadhaa Lissu ameishutumu Idara ya Usalama wa Taifa sio tu kumhujumu yeye na chama chake bali pia kuihusisha na jaribio dhidi ya maisha yake Septemba 2017.