Ujio wa Mama @SuluhuSamia 2.0: Kutoka Twiti ya Uzushi Iliyozua Taharuki Kuhusu Afya Yake Hadi Hotuba Iliyojaa Mamlaka Na Kukumbusha "Mimi Ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
Kwenye historia na maendeleo ya mtandao wa intaneti, kuna zama zinazojulikana kama Web 1.0, Web 2.0, Web 3.0 na Web 4.0.
Bila kuingia kwa undani na pengine kuwachanganya, Web 1.0 ni zama ya awali ya intaneti ambayo ilihusisha kusoma tu kilichowekwa mtandaoni (read-only web).
Web 2.0 iliwezesha kusoma na kuandika (read-write web). Hiki ndicho kipindi mtum…