#UziwaTwita Kuikaribisha Julai Na Neno Kuhusu #Uchaguzi2020
Kwanza, nina furaha kuwajulisha kuhusu ujio wa jarida la mtandaoni la JASUSI ambalo litajikita zaidi kuhusu masuala ya intelijensia. Vilevile litagusia masuala ya usalama wako mtandaoni na kukufundisha mbinu mbalimbali za kuwa salama. Kupitia jarida hilo natarajia pia kuendesha kozi ya awali ya udukuzi wa kimaadili. Nitawaletea maelezo zaidi hivi punde.