Wasifu wa shushushu mzoefu Noordin Haji, aliyeteuliwa na Rais Ruto kuchukua nafasi ya Philip Kameru kama mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya (NIS), huku akisubiri kuidhinishwa na Bunge.
Nairobi, Kenya: Rais William Ruto amemteua Mwendesha Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kushika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya, NIS.
Haji, ambaye licha ya kuwa shushushu mzoefu miaka ya nyuma, pia aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa NIS, anasubiri kuidhinishwa na Bunge la nchi hiyo, kuchukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa n…